SIMBA KAMILI KUWAVAA WAARABU KIMATAIFA

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye anga la kimataifa Simba wameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo wao wa hatua ya makundi dhidi ya wapinzani wao SC Sfaxine utakaopigwa nchini Tunisia.

Ipo wazi kwamba kwenye mchezo waliokutana Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 Simba walishinda kwa mabao 2-1 na mtupiaji alikuwa mkandaji Kibu Dennis ambaye yupo kwenye msafara uliowasili Tunisia kwa maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo muhimu.

Safari ya Simba kuelekea Tunisia ilianza Januari Mosi 2025 na wakatua Istanbul, Uturuki kisha safari ikaendelea mpaka Tunisia walipowasili salama kwa maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo muhimu.

Ni wachezaji 22 wapo katika msafara wenye jumla ya watu 50i ikiwa ni viongozi na benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Miongoni mwa wachezaji hao ni Ladack Chasambi, Che Malone, Mohamed Hussen, Yusuph Kagoma, Kibu Dennis, Mousa Camara ambaye ni kipa namba moja wa Simba.

Januari 5 2025 Simba itakuwa ugenini kwenye kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya SC Sfaxine katika hatua ya makundi, Kombe la Shirikisho Afrika.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa lakini wapo tayari kwa kupata matokeo mazuri.

“Ni mchezo mgumu ambao tunakwenda kucheza na tunatarajia kwamba tutapata ushindani mkubwa ila tupo tayari kuona tunapata matokeo mazuri kwani kila kitu kipo kwenye mpango kazi wake.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.

Happy new year 2025.