LIVERPOOL MOTO HAUZIMI, SALAH NI MWENDO WA REKODI

WAKIWA ugenini Liverpool walikomba pointi tatu muhimu dhidi ya Tottenham kwa ushindi wa mabao 6-3 mchezo wa Ligi Kuu England ambapo moto wao sasa hauzimi kutokana na mwendelezo wa kusaka ushindi ndani ya uwanja.

Mabao ya Diaz alitupia mara mbili dakika ya 85, 23, Mohamed Salah dakika ya 54, 61, Szoboszlai dakika ya 45 na Mac dakika ya 36. Salah ameandika rekodi ya kufunga mabao mawili na pasi mbili za mabao kwenye mchezo huo muhimu.

Tottenham sio kinyonge walitupia kupitia Solanke dakika ya 83, Kukuveski dakika ya 72 na Maddison dakika ya 41.

Liverpool nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 16 ikiwa na pointi 39 kibindoni safu ya ushambuliaji imetupia mabao 37.

Chelsea ni namba mbili pointi 35 baada ya kucheza mechi 17 na safu ya ushambuliaji imetupia mabao 37.

Tottenham sasa imecheza mechi 17 ikiwa na pointi 23 nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Engand huku mabingwa watetezi Man City nafasi ya 7 pointi 27 baada ya kucheza mechi 17.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.