MWAMBA Aboutwalib Mshery kipa wa Yanga leo Desemba 22 ana kibarua cha kutimiza majukumu yake mbele ya Wajelajela, Tanzania Prisons mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex.
Huu unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Mshery kuanza kikosi cha kwanza msimu wa 2024/25 huku Kibwan Shomary ambaye mchezo uliopita dhidi ya Mashujaa alitoa pasi yake ya kwanza ya bao akianza ndani ya kikosi cha kazi cha Yanga.
Hiki hapa kikosi cha kwanza:-
Aboutwalib Mshery, Kibwana, Kibabage, Dickson Job, Bacca, Khalid Aucho, Farid Mussa, Mudathir, Dube Prince, Aziz Ki, Mzize.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.