KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davids ameweka wazi kuwa kuna ushindani mkubwa ndani ya uwanja jambo ambalo wanafanya kazi kila wakati kuhakikisha wanakuwa bora wakiwa kwenye hesabu za kucheza ugenini kimataifa mchezo ujao.
Fadlu amekiongoza kikosi cha Simba katika mechi 11 za ligi ushindi mechi 9, sare moja na kichapo ilikuwa dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa katika mchezo wa kimataifa ilikuwa Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 1-0 Bravos bao likifungwa na Jean Ahoua kwa pigo la penalti.
“Ushindani ni mkubwa na kila timu inapambana kupata matokeo, nawapongeza wachezaji wanajituma na kufuata maelekezo kuna vitu vidogo vya kufanyia kazi.”
Kibindoni ni pointi 28 na safu ya ushambuliaji imetupia mabao 22 kinara ni Jean Ahoua mabao matano na pasi nne akihusika katika mabao 9.
Vinara ni Azam FC pointi 30 baada ya kucheza mechi 13 2024/25 mchezo wa fungua Desemba kwa Azam FC ilikuwa ugenini dhidi ya Dodoma Jiji ilikomba pointi tatu mazima na ubao ulisoma Dodoma Jiji 1-3 Azam FC.
Mchezo ujao kwa Simba itakuwa kimataifa katika Kombe la Shirikisho Afrika unatarajiwa kuchezwa Desemba 8 2024 watakuwa kwenye msako wa pointi tatu muhimu dhidi ya CS Constantine.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.