MERIDIANBET YAISHIKA MKONO HOSPITALI YA NDUMBWI MBEZI

Meridianbet wamefanikiwa kuhakikisha wanarudisha kwenye jamii yao ambayo mara kwa mara wamekua wakiwaunga mkono, Ambapo leo wamefika eneo la Mbezi ya Juu na kutoa msaada wa vifaa vya usafi kwa Hospitali.

Mabingwa hao wa michezo ya kubashiri wamekua kwenye utaratibu huu kwa miaka mingi wakihakikisha wanagawana na jamii yao kila ambacho wamekivuna, Hii imewafanya kwa mara nyingine kurejea kutoa vifaa vya usafi kwenye hospitali ya Ndumbwi inayopatikana Mbezi.

Hospitali ya Ndumbwi kwa mara ya kwanza inapokea msaada wa vifaa vya usafi kutoka kwa mabingwa wa michezo ya kubashiri mapema, Huku wakionesha kufurahishwa na jambo hilo lililofanywa na kampuni ya Meridianbet.

Bado mabingwa wa michezo ya kubashiri Meridianbet wanaendelea kuhakikisha unapigwa mkwanja wa kutosha kupitia michezo mbalimbali inayopigwa haswa michuano ya ligi ya mabingwa ulaya inayopigwa katikati ya wiki hii ambapo wanaendelea kumwaga ODDS BOMBA kila siku.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Masoko ndani ya Meridianbet alipata nafasi ya kuzungumza machache katika hafla hiyo “Tunatambua umuhimu wa usafi wa mazingira maana usafi ni afya ndio maana leo tumeweza kuleta vifaa hivi katika hospitali hii kwa dhumuni la kuimarisha usafi katika mazingira ya hospitali na kuondokana na magonjwa yatokanayo na uchafu”.

Aidha Diwani wa eneo la Mbezi Juu Bi Anna Lukindo ambaye alikuepo kwenye tukio hilo alipata nafasi ya kuzungumza machache juu ya jambo hilo la kiungwana lililofanyika “Kiukweli nipende kuwashukuru Meridianbet kwa kufika katika hospitali yetu ya Ndumbwi na kuweza kutoa vifaa vya usafi ambavyo vitasaidia kuhakikisha mazingira ya hospitali yetu yanakua makazi, Niwape pongezi kwa jambo hilo wasiishie hapa tu waendelee kuwashika mkono na wengine”