HIKI HAPA KIKOSI CHA TAIFA STARS KUFUZU CHAN

Kocha ambaye atakiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ya wachezaji wa Ligi ya ndani Bakar Shime, ameita wachezaji kwa ajili ya mchezo wa kwanza dhidi ya Sudan ambao unatarajiwa kuchezwa Oktoba 27, 2024 nchini Mauritania.

Shime amesema, ameita wachezaji wengi kutoka timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ ilikuendelea kuwapa uzoefu lakini vilevile kuhakikisha Ligi haitosimama kwa sababu baadhi ya klabu kuwakosa wachezaji wake muhimu.

“Tumeita kikosi cha Taifa cha wachezaji wa ndani tukiwa na malengo kuwa ligi yetu lazima iendelee hivyo tumeita wachezaji ambao hawatafanya ligi isimame lakini pia kupata matokeo mazuri katika mchezo wetu wa kwanza ambao tutacheza dhidi ya Sudan kule nchini Mauritania.”

– Bakari Shime, Kocha wa timu ya taifa ya CHAN.