HIZI HAPA MECHI ZIJAZO ZA YANGA NA SIMBA

BAADA ya Kariakoo Dabi kugota mwisho mzunguko wa kwanza na ubao wa Uwanja wa Mkapa Oktoba 19 kusoma Simba 0-1 Yanga kazi bado inaendelea kwa Ligi Kuu Bara mechi kuwa za moto huku vinara wakiwa ni Singida Black Stars ambao walikomba pointi tatu kwenye mchezo uliopita dhidi ya Namungo.

Oktoba 20 ubao wa Uwanja wa Liti baada ya dakika 90 ulisoma Singida Blacks Stars 2-0 Namungo mabao yakifungwa na Marouf Tchakei yote mawili ilikuwa dakika ya 55 na dakika ya 86 kwa mkwaju wa penalti.

Ikumbukwe kwamba bao la ushindi la Yanga kwenye Kariakoo Dabi lilifungwa na Maxi Nzengeli dakika ya 86 ikiwa zimesalia dakika 4 Kariakoo Dabi kugota mwisho hizi hapa mechi zijazo kwa Yanga ambao ni mabingwa watetezi na Simba namna hii:-

Mechi za Yanga

JKT Tanzania unatarajiwa kuchezwa Oktoba 22 Uwanja wa Azam Complex
Coastal Union, Oktoba 26 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Singida Black Stars, Oktoba 30 Uwanja wa New Amaan

SIMBA
Tz Prisons, Oktoba 22 Uwanja wa Sokoine
Namungo Oktoba 25 Uwanja wa KMC Complex
JKT Tanzania Oltoba 29 Uwanja wa KMC Complex

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.