AZAM FC YABADILI MUELEKEO, KOCHA AFICHUA SIRI

BAADA ya kukomba pointi tatu muhimu kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Mbeya, Uwanja wa Sokoine Kocha Mkuu wa Azam FC Rachid Taoussi amefichua kuwa walibadili muelekeo kulingana na mchezo husika na kupata matokeo kama ambavyo walifanya vizuri mazoezini.

Oktoba 18 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Sokoine ulisoma Tanzania Prisons 0-2 Azam FC mabao yalifungwa na Nado  na Saadun.

Kocha amesema kuwa ilikuwa kazi ngumu kwenye mchezo huo kutokana na ushindani ambao ulikuwa kwa timu zote mbili na mwisho wakapata ushindi jambo ambalo lilikuwa ni muhimu kwao.

“Tulianza vizuri kwenye mchezo wetu na haikuwa rahisi kwa kuwa tulikuwa na tunacheza na timu ambayo ilikuwa inatafuta matokeo mwisho tukafanikiwa kupata ushindi kipindi cha kwanza baada ya kubadilisha muelekeo.

“Kikubwa ni kufanya vizuri kwenye uwanja wa mazoezi unaona namna ambavyo wachezaji wamecheza na kutafuta matokeo ni namna ambavyo tulikuwa na mazoezi mazuri, hivyo mchezo wa mpira unatoa matokeo kulingana na mazoezi ya siku husika na imekuwa nzuri kwetu kupata ushindi.”

Azam FC inafikisha pointi 15 baada ya kucheza mechi 8 safu yake ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 8 kwenye msimamo ipo nafasi ya pili.

USIPANGE kukosa kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, hii ni simulizi iliyaoandikwa na Mtunzi Lunyamadzo Mlyuka, A Boy From Njombe, kuipata 0756 028 371.