KAYOKO APEWA MECHI YA KESHO, SIMBA vs YANGA KWA MKAPA

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imemtangaza mwamuzi Ramadhan Kayoko kutoka Dar es Salaam kuwa refa atakayesimamia sheria 17 za mchezo wa soka kwenye Derby ya Kariakoo itakayopigwa Jumamosi, Oktoba 19, 2024 katika dimba la Benjamin Mkapa.

Kayoko atasaidiwa na Mohamed Mkono kutoka Tanga na Kassim Mpanga kutoka Dar es Salaam, huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Tatu Malogo katika mchezo huo utakaopigwa kesho majira ya saa 11:00 jioni.