>

JONAS MKUDE AFUNGUKIA KARIAKOO DABI

LEGEND Jonas Mkude anayekipiga ndani ya kikosi cha Yanga amesema kuwa hana hofu na Kariakoo Dabi kutokana na uzoefu alionao muda wowote yupo tayari kuchezwa kwani hiyo ni kazi yake.

Ikumbukwe kwamba Mkude ni timu mbili kubwa amecheza kwa sasa katika ardhi ya Tanzania, alianza na Simba kisha akaibukia Yanga baada ya kukutana na Thank You Simba.

Oktoba 19 2024 mchezo wa Kariakoo Dabi kati ya Simba na Yanga unatarajiwa kuchezwa ikiwa ni mzunguko wa kwanza kwa wababe hao kukutana uwanjani katika ligi inayodhaminiwa na NBC ambao ni wadhamini wakuu na matangazo ni Azam TV ambao wataurusha mchezo huu mubashara.

Mkude amesema kila wakati wanafanya maandalizi kwa ajili ya mechi zao zote ikiwa ni pamoja na mchezo dhidi ya Simba kwa kuwa upo kwenye ligi.

“Kuhusu Kariakoo Dabi naona ni mchezo wenye ushindani mkubwa lakini sina hofu kucheza yaani muda wowote nipo tayari kwa kuwa ni maisha yangu kucheza mpira sina hofu na ninatambua kwamba mpira ni kazi ambayo ninaifanya kwa namna yoyote mashaka hapana.

“Mazoezi na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi ni kitu muhimu na tunashirikiana wachezaji wote, benchi la ufundi linatambua nani anapaswa kuanza na kipi kinapaswa kufanyika kuelekea kwenye mchezo huo.”

Yanga imecheza mechi nne za ligi ambazo ni dakika 360 ikikomba pointi tatu kila mchezo na kufikisha jumla ya pointi 12 kibindoni ni mabingwa watetezi wa ligi.

USIKOSE kusoma kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, mtunzi Lunyamadzo Mlyuka, kukipata 0756, 028 371.

Njombe kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari kama unaelekea IFM, Kigamboni.