>

MANCHESTER CITY YASHINDA KESI YAKE DHIDI YA BODI YA LIGI KUU

Klabu ya Manchester City ya Uingereza Oktoba 7, 2024 imeshinda kesi yake dhidi ya Bodi ya Ligi Kuu nchini humo ya sheria ya matumizi ya fedha iliyokuwa inawahusisha wamiliki wa klabu hiyo.

Klabu hiyo inayomilikiwa na Abu Dhabi United Group, kampuni inayomilikiwa na familia ya kifalme ya Abu Dhabi iliyo chini ya Sheikh Mansour ilishtakiwa na malalamiko yaliyokuwa yanahusisha uvunjaji wa vipengele vya sheria ya matumizi ya fedha.

Manchester City wametoa tamko la kudai ushindi dhidi ya Ligi Kuu kufuatia kesi yao ya kisheria dhidi ya kanuni za Associated Party Transaction (ATP), huku ligi hiyo pia ikiwa imetoa taarifa inayoashiria sheria za ATP zinahitajika ili kuendelea kudhibiti shughuli za kifedha kwa vilabu vyake.

Mahakama huru imegundua kuwa baadhi ya kanuni za Ligi Kuu hazikuwa halali kuhusiana na kanuni za ATP, kwani Man City pia ilitaja mikataba miwili ya udhamini ambayo Benki ya First Abu Dhabi na Etihad Aviation Group haikuidhinishwa na Ligi.

Manchester City imesema jopo hilo liligundua sheria za APT “hazikutenda haki kimuundo” na kwamba jopo hilo liliweka kando maamuzi maalum ya Ligi Kuu ya Uingereza kuelezea tena thamani ya soko ya haki ya miamala miwili iliyoingiwa na kilabu ambayo ni mkataba na Benki ya First Abu Dhabi na Etihad Aviation Group.