>

MUIGIZAJI MKONGWE KUTOKEA MAREKANI JOHN AMOS AMEFARIKI DUNIA

Muigizaji Mkongwe kutokea Marekani John Amos (84), amefariki dunia.

Mtoto wa marehemu Bw. Kelly Amos amethibitisha kuwa baba yake alifariki Agosti 21 jijini Los Angeles.

Bado haijafahamika ni kwanini taarifa za kifo chake zimechelewa kutolewa.

Aidha, Binti wa Marehemu Bi. Shannon Amos ameeleza kuwa taarifa za kifo cha baba yake amezipatia kwenye mtandao.

Amos alijipatia umaarufu kwa kuigiza katika filamu mbalimbali zikiwemo “Coming to America” , “Roots” na “Die Hard 2” ,akifanya kazi na watu mashuhuri kama Sylvester Stallone na Bruce Willis.

Kabla ya kuingia kwenye tasnia ya filamu, Amos alicheza mpira wa kulipwa katika ligi kadhaa za nchini Marekani.