>

RATIBA LIGI KUU BARA BONGO HII HAPA

MWENDO wa msako wa ushindi ndani ya uwanja kwenye mechi za Ligi Kuu Bara unatarajiwa kuendelea leo Septemba 27 kwa mchezo mmoja kuchezwa Uwanja wa Tanzanite na utarushwa mubashara Azam TV  hivyo kama utashindwa kwenda uwanjani ni muda wako kukaa kwenye kideo kutazama mubashara.

Ikumbukwe kwamba Septemba 26 2024 dunia ilishuhudia Mzizma Dabi Uwanja wa New Amaan Complex baada ya dakika 90 ilikuwa Azam FC 0-2 Simba na mabao yakifungwa na Leonel Ateba na Fabrince Ngoma.

Leo Septemba 27 mchezo mmoja unatarajiwa kuchezwa itakuwa ni Fountain Gate dhidi ya Kagera Sugar itakuwa saa 10: oo jioni mchezo huu utachezwa.

Septemba 28 2024 kutakuwa na mechi za kutosha ambapo ratiba inatarajiwa kuwa namna hii:-

Ken Gold ambayo imetoka kupoteza mchezo wake dhidi ya Yanga hii itamenyana na Tabora United itakuwa saa  8:00 mchana.

Coastal Union v Pamba Jiji itakuwa saa 10:15 jioni

Namungo v Tanzania hii itachezwa saa 1:00 usiku.