>

SERGIO RICO AJIUNGA NA KLABU YA AL GHARAFA YA QATAR

Aliyekuwa golikipa wa klabu ya Paris Saint German, Sergio Rico amejiunga na klabu ya Al Gharafa ya Qatar kama mchezaji mpya klabuni hapo kwa uhamisho huru baada ya kuondoka PSG.

Rico (31) raia wa Uhispania amekuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya mwaka mmoja baada ya kupata jeraha baya la kichwa katika ajali ya kuanguka kutoka kwenye farasi mnamo Mei 2023.

Rico amewahi kuitumikia klabu hiyo Fulham kwa mkopo kutoka Sevilla msimu wa 2018-19 kabla ya kujiunga na PSG msimu wa 2020-21 na kudumu klabuni hapo mpaka Juni 30, 2024 mkataba wake ulipofikia ukomo.