Simba mabao yamefungwa na Kibu Dennis dakika ya 36. Ateba dakika ya 45 bao la dakika ya 63 limefutwa kwa kile kilichoelezwa kuwa mfungaji alikuwa eneo la kuotea.
Bao la tatu limefungwa na Edwin Balua dakikaya 89 ikiwa ni tiketi ya Simba kutinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.
KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids kipo kwenye msako wa tiketi ya kutinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Mkapa mbele ya mashabiki wake wengi waliojitokeza kushuhudia burudani hiyo.
Dakika 45 za mwanzo ubao wa Uwanja wa Mkapa umesoma Simba 2- 1 Al Ahli Tripoli ambapo ni wageni walianza kupata bao mapema kupitia kwa mshambuliaji wao mwenye rasta kama za Kibu Dennis wa Simba.
Bao la Al Ahli Tripoli limefungwa na Cristovao Mabululu dakika ya 17 likiwa ni bao la mapema zaidi kwa wapinzani hawa wawili ndani ya uwanja kwenye anga la kimataifa.
Kwa upande wa Simba ni rasta Kibu Dennis alianza kufunga kwenye anga la kimataifa dakika ya 36 na Ateba Leonel akifunga dakika ya 45.
Mshindi wa jumla mchezo wa leo anatinga hatua ya makundi kwenye kombe la Shirikisho Afrika huku Simba wakiwa na chaguo moja kushinda mchezo wa leo kwa namna yoyote kusonga mbele.