>

AZAM FC WAMEANZA NAMNA HII NA BENCHI JIPYA

BENCHI jipya la ufundi la Azam FC mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Bara limeshuhudia wakigawana pointi mojamoja dhidi ya wapinzai wao Pamba Jiji katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Septemba 14 2024.

Ikumbukwe kwamba mchezo wa kwanza wa ligi msimu wa 2024/25 ilikuwa JKT Tanzania 0-0 Azam FC wakati huo timu ilikuwa chini ya Yusuph Dabo ambaye alipewa mkono wa Thank You pamoja na benchi lake zima la ufundi.

Ni Rachid Taoussi alitangazwa kuwa kocha mpya wa timu hiyo na alikuja na benchi lake lenye wasaidizi watatu, kocha msaidizi, Badr Driss, kocha wa utimamu wa mwili, Ouajou Driss na kocha wa makipa, Rachid El Mekkaoui.

Katika mchezo huo beki Cheikh Sidibe alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 72 baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano na mwamuzi wa mchezo huo.

Kocha Taoussi amesema:”Wachezaji walifanya kazi kubwa na walicheza vizuri kipindi cha kwanza, makosa ambayo yametokea tutayafanyia kazi kwa ajili ya mechi zijazo.”

Dakika 180 Azam FC imekusanya pointi mbili kwenye msako wa pointi sita imeyeyusha pointi nne ndani ya uwanja safu ya ushambuliaji ikiwa haijafungua akaunti ya mabao na ulinzi haujafungwa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Dizo Click.