BAADA ya mchezo wa Septemba 14 2024 ubao kusoma CBE SA 0-1 Yanga dakika 90 za kazi zinatarajiwa kuchezwa Jumamosi katika ardhi ya Tanzania.
Chini ya MiguelGamondi ambaye ni kocha mkuu wa Yanga katika dakika 90 za ugenini bao la ushindi lilipachikwa na mshambuliaji Prince Dube dakika ya 45.
Gamondi ameweka wazi kuwa kuanza kwa ushindi ugenini ni jambo ambalo limewapa nguvu kuelekea kwenye mchezo wa pili ambao utakuwa na ushindani mkubwa.
“Tumepata ushindi ugenini hilo lipo wazi hivyo kuelekea kwenye mchezo wetu tukiwa nyumbani tunaamini kwamba tutafanya kazi kubwa ili kupata matokeo chanya. Makosa tutafanyia kazi kwa ajili ya mchezo wetu ujao.”
Mchezo ujao kwa Yanga unatarajiwa kuchezwa Septemba 21 siku ya Jumamosi Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Tayari kikosi cha Yanga kimerejea salama Dar baada ya kukamilisha kazi kwenye mchezo wao uliopita wakiwa ugenini.