FUNGAFUNGA: CHAMA NI MCHEZAJI MZURI

MICHAEL Fred, fungafunga mshambuliaji wa zamani wa Simba amesema kuwa mchezaji Clatous Chama ni miongoni mwa wachezaji wazuri aliopata nafasi ya kucheza nao kwenye ligi.

Kwa sasa Chama yupo ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi alipata nafasi ya kucheza mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaiataba baada ya dakika 90 ilikuwa Kagera Sugar 0-2 Yanga.

Kwenye mchezo huo Chama alianzia benchi aliingia kipindi cha pili kwenye msako wa pointi tatu katika mchezo wa kwanza wa ligi walikomba pointi tatu ugenini.

Akizungumza na Saleh Jembe, Fred maarufu kwa jina la fungafunga amesema kuwa miongoni mwa wachezaji wenye uwezo mzuri ndani ya uwanja kwa kuwa nilicheza.

“Chama ni mchezaji mzuri nilipata nafasi ya kucheza naye ndani ya Simba nakumbuka kwenye Kariakoo Dabi alinipa pasi ambayo nilifunga bao kwenye mchezo huo hivyo nilifurahi kucheza naye na kwa sasa maisha yanaendelea.”