WANASIMBA WAITWA KMC COMPLEX KUPATA BURUDANI

AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa Wanasimba wasikubali kukaa nyumbani Agosti 31 2024 timu hiyo itakapokuwa ikicheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Al Hilal ya Sudan.

Leo timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids inatarajiwa kutupa kete hiyo ya kimataifa saa 10:00 jioni.

Ally amebainisha kuwa ni mchezo mzuri utakaowapa furaha mashabiki wa Simba kwa kuwa wachezaji wanapenda kutimiza majukumu yao wakiwa uwanjani.

“Wanasimba ni mchezo wetu wa kimataifa hivyo usikubali kukaa nyumbani njoo uishuhudie Simba ya ubaya ubwela na inaongeza pumzi ya moto hii sio ya kukosa kwa kweli kwa kuna kitu kimeongezeka.

“Usifikiri kwa kuwa uliiona Simba ikicheza na Fountain Gate mchezo wake uliopita ukadhani umemaliza hapana kuna kazi kubwa inakwenda kufanyika na wachezaji wapo tayari mashabiki mjitokeze kwa wingi mpate burudani.”

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye kikosi cha Simba kwa sasa ni Kibu Dennis, Awesu Awesu, Hussen Abel, Aishi Manula.