MATAJIRI wa Dar, Azam FC wametinga hatua ya fainali Ngao ya Jamii kwa ushindi wa mabao 5-2 Coastal Union katika hatua ya nusu fainali.
Ni Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar nusu fainali ya kwanza imechezwa anasubiriwa mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Yanga na Simba, Uwanja wa Mkapa
Sillah alipachika bao dakika ya 13, Feisal Salum dakika ya 49, Blanco dakika ya 45, Adam Adam dakika ya 87 na Meza dakika ya 90 kwa Coastal Union ni Semfuko dakika ya 27 na Hassan dakika ya 86.
Kwa mujibu wa kiungo Feisal ameweka wazi kuwa wao wapo tayari kucheza na timu yoyote kwenye hatua ya fainali kwa kuwa kila timu ina kazi kwenye mchezo wake husika.