MAXI NZENGELI AWATUNGUA SIMBA NGAO YA JAMII

YANGA wametumia dakika 44 kuwaadhibu Simba katika Ngao ya Jamii mchezo wa nusu fainali Uwanja wa Mkapa kukiwa na dakika 45 za kipindi cha pili zimebaki.

Maamuzi ya haraka kwa wachezaji wa Yanga katika kutoa pasi yamewapa wakati mgumu Simba katika eneo la ulinzi linaloongozwa na Che Malone Fondoh.

Bao la kuongoza ni mali ya Maxi Nzengeli ambaye alifanya majaribio mawili hayakuwa chanya kutokana na kipa Mousa kuokoa na moja kutoka nje.

Mshindi wa jumla atakutana na Azam FC katika fainali Agosti 11 Uwanja wa Mkapa.