KUELEKEA kwenye mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii kati ya matajiri wa Dar, Azam FC dhidi ya Wagosi wa Kaya, kutoka Tanga, Coastal Union maofisa habari wa timu zote mbili wamepigana mikwarakwa kubainisha kuwa wote wanahitaji ushindi.
Kwenye mchezo wa leo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar mshindi atakutana na Yanga ama Simba ambao nao watakuwa na kazi ya kusaka ushidi Uwanja wa Mkapa ambapo fainali inatarajiwa kuchezwa Agosti 11 2024.
Ibwe amesema:”Tuna wakati mzuri Zanzibar na tunaamini tutakuwa na mchezo mzuri dhidi ya Coastal Union ambao wanastahili kuwa katika hatua hii lakini sisi tunahitaji kusonga mbele.
“Wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo wa nusu fainali dhidi ya wapinzani ambao tunatambua ubora wao kwa kuwa tumekutana nao kwenye mechi za ushindani, tupo tayari kwa ajili ya kupata matokeo.”
Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye kikosi cha Azam FC ni Yanick Bangala, Feisal Salum, Nado.
Abbas El Sabri, Ofisa Habari wa Coastal Union ameweka wazi kuwa huwa kutakuwa na ugumu mkubwa wakikutana Azam FC dhidi ya Coastal Union.