MASHABIKI NANE WA SOKA KWENDA DUBAI KUPITIA PROMOSHENI YA PARIMATCH NA AIRTEL

JUMLA ya mashabiki nane wa soka watapata fursa ya kutembelea nchini Dubai endapo watashinda tiketi kupitia promosheni ya Dubai Kumenoga ilitoziduliwa na Kampuni ya michezo ya kubahatisha Parimatch kwa kushirikiana na Airtel Tanzania  kupitia huduma za Airtel Money.

Promosheni hiyo ni muendelezo wa kampeni kubwa iliyomalizika ya Zigo la Euro 2024 nchini Ujerumani ambapo mashabiki wa soka  walishinda zawadi mbalimbali.

Meneja Masoko wa Parimatch, Levis Paul alisema kuwa dhumuni kubwa ya promosheni hiyo ni kuwapa wateja wa Parimatch thamani na kukata kiu ya ndoto za Watanzania wanaotamani kusafiri kwenda Dubai kwa mapumziko.

“Promosheni hii ni mahususi kwa wateja wetu wote wa Parimatch na wanaotumia mtandao wa Airtel Money wenye akaunti na hata wateja wapya watakaojiunga kwa sasa.

Lengo letu  ni kuwawezesha kuendelea kucheza na kufurahia burudani kabambe za falme za kiarabu (Dubai). Kuanzia Agosti 7 mpaka Oktoba 6, mteja wa Parimatch akifanya ubashiri wake kwenye mchezo wowote wa soka kupitia tovuti  www.parimatch.co.tz au App yetu ataingia kwenye droo na kuweza kushinda tiketi,” alisema Levis.

Alisema kuwa vilevile kwa asiyekuwa mteja  wao anaweza kushiriki kwa kujisajili kupitia www.parimatch.co.tz na kuweka pesa kupitia airtel money na kuweka ubashiri katika mechi yeyote.  Kadri unavyoweka beti zaidi ndivyo unajiongezea nafasi ya kujishindia tiketi ya kwenda Dubai au kujishindia pesa taslimu kiasi cha Sh50,000 kila siku hadi Sh200,000” alisema Levis.

Levis pia alisema kuwa mteja anaweza kujisajili kupitia menu ya Airtel Money, mteja anaweza kufuata njia hizi ili kuweza kuweka pesa yake na kuanza kusuka mkeka wa ushindi *150*60# kisha namba 4 lipa bill, weka code za 351144 unaweza kuweka pesa na kushinda kushinda safari ya kwenda Dubai au pesa taslimu kutoka katika droo ya siku husika ya promosheni

Pamoja na hayo, Levis amewataka Watanzania kiujumla kuchangamkia fursa hiyo ya kipekee kwa kubeti na Parimatch ili wawe miongoni mwa washindi watakaobahatika kujishindia safari ya kupelekwa Dubai na Parimatch kula bata huku gharama zote zikiwa zimelipiwa.

Kampuni ya Parimatch ndio kinara wa michezo ya kubashiri mtandaoni na imekuwa ikitoa ofa kubwa ya bonasi ya Ukaribisho ya 125% hadi kufikia TZs 1,000,000 kwa wateja wapya wanaojiunga nao!

Parimatch imekuwa ikifanya kazi nchini Tanzania tangu mwaka 2019, ikitoa huduma nzuri ikijumuisha malipo ya haraka, odds kubwa na promosheni za kusisimua kwenye soka, Kasino na Michezo ya virtual. Mbali na soka, kampuni ya Parimatch pia hutoa mamia ya matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, mpira wa vikapu, Kriketi, baseball na michezo mingine mingi ya Live na pre-match.