KAZI inaendelea ambapo tamasha lingine kubwa linatarajiwa kufanyika Uwanja wa Liti, Singida ikiwa ni utambulisho wa wachezaji wapya na benchi la ufundi.
Ni Singida Black Stars wameweka wazi kuwa kutakuwa na burudani kubwa katika kilele cha Big Day,Uwanja wa Liti Agosti 10 2024 ambapo kutakuwa na mchezo wa kirafiki utakaokuwa na ushindani mkubwa.
Hilo ni Vibe la Chui itakuwa siku hiyo ambapo kutakuwa na mchezo wa kitaifa wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir ya Burundi na utambulisho wa wachezaji wapya kuelekea msimu wa 2024/25.
Ofisa Habari wa Singida Black Stars, Hussen Masanza amesema: “Ni siku ambayo itakuwa ya kipekee zaidi ukizingatia kwamba tumeona namna matamasha yaw engine yalivyokuwa nina amini mashabiki watakaojitokeza watapata burudani iliyo bora.’