AZAM FC YAPATA MRITHI WA SURE BOY ALIYESAINI YANGA

KIUNGO wa mpira Ibrahim Ajib baada ya kusitisha mkataba wake na mabosi wake wa zamani Simba ametambulishwa ndani ya kikosi cha Azam FC.

Ajib alikuwa akicheza ndani ya kikosi cha Simba lakini hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza jambo ambalo limewafanya mabosi wake kuamua kusitisha mkataba wake.

Ni dili la mwaka mmoja amesaini ndani ya Azam FC kuweza kuwatumikia mabosi wa Dar.

Amekabidhiwa jezi namba 8 iliyokuwa inavaliwa na Sure Boy ambaye amesaini dili la miaka miwili ndani ya kikosi cha Yanga.