MAYANGA:TUNAPAMBANA KWA AJILI YA TIMU

VITALIS Mayanga mshambuliaji namba moja wa Polisi Tanzania amesema kuwa wanapambana kwenye kila mechi ili kuwea kupata matokeo chanya kwa ajili ya timu.

Polisi Tanzania imekuwa kwenye mwendo mzuri msimu wa 2021/22 huku Mayanga akiwa amejenga ushkaji na nyavu kwa kuwa amekuwa akifunga na kutengeneza pasi za mabao.

Ikiwa imecheza mechi 11 na kufunga mabao 11 na pointi zake ni 17 Mayanga amehusika kwenye mabao nane ambapo amefunga matano na kutoa pasi tatu za mabao.

Nyota huyo mzawa amesema:”Tunapambana kwa ajili ya timu na kikubwa ni kuona kwamba timu inashinda kwenye kila mchezo ambao tunacheza kwenye ligi.

“Ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji kushinda kwa namna yoyote ile hivyo tutaendelea kupambana ili kupata ushindi,”.