KLABU ya KMC kwa msimu wa 2021/22 kwenye mechi zao mbili za vigogo ndani ya ligi hawajawa na bahati ya kusepa na pointi tatu zaidi walikuwa wakiambulia maumivu ya kunyooshwa.
Ikumbukwe kwamba KMC makazi yao yapo Dar lakini kwa mechi zilizokuwa zikiwakutanisha dhidi Yanga na Simba walikuwa wakizipeleka nje ya Dar.
Ilikuwa ni ile dhidi ya Yanga iliyochezwa Uwanja wa Majimaji, Songea, Oktoba 19, ubao ulisoma KMC 0-2 Yanga na ule wa pili ilikuwa dhidi ya Simba ulichezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora Desemba 24 na ubao ulisoma KMC 1-4 Simba.
Katika mechi mbili ambazo ni dakika 180 walizocheza nje ya Dar KMC imeyeyusha pointi sita mazima huku ikifungwa jumla ya mabao saba na ni bao moja safu yake ya ushambuliaji ilifunga.
Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala aliliambia Championi Jumatatu kuwa sababu kubwa ya kupeleka mechi nje ya Dar ni kuweza kuwafikia mashabiki wao.
“Tunamashabiki wengi ambao wanaitambua KMC lakini wanahitaji kuiona, kuhusu matokeo ni suala ambalo linatokea na tunaamini kwamba benchi la ufundi litafanyia kazi mapungufu,” .