>

MTIBWA SUGAR KUIKABILI YANGA

MTIBWA Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu,Zuber Katwila ina kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ikiwa itapata ushindi kwenye mchezo wa leo itafikisha pointi 71 ikizidi kuwa namba moja na kufikia pointi zitakazowapa ubingwa.

Itakuwa ni ubingwa wa 30 kwa Yanga ndani ya ligi ikiwapoteza wapinzani wake wakubwa Azam na Simba ambao wanapambania nafasi ya pili kwa sasa.

Mtibwa Sugar yenyewe inapambana kwenye kufufua matumaini ya kucheza play off kutokana na kutokuwa na mwendo mzuri ndani ya ligi.

Kibindoni ina pointi 20 msimu wa 2023/24 ukiwa na ushindani mkubwa kwenye vita ya timu ambazo zitashuka daraja na zile ambazo zitabaki ndani ya ligi.

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amebainisha kwamba timu hiyo inahitaji maombi kupata matokeo kwenye mechi zake ambazo zimebaki.