SIMBA YATINGA FAINALI, NGOMA NI BALAA

MWAMBA Fabrice Ngoma na Zanzibar ni damudamu kutokana na kuwa katika kiwango bora kama ambavyo ilikuwa kwenye Mapinduzi 2024 alipoibuka mchezaji bora katika Michuano hiyo.

Hivyo nyota huyo kwenye uwanja eneo la kiungo amekuwa na balaa zito wakiwa visiwani jambo linalofanya akombe tuzo hizo mara kwa mara.

Kwa mara nyingine tena Simba wamerejea Zanzibar, Uwanja wa New Amaan Complex wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KVZ, Ngoma kawa mchezaji bora wa mchezo.

Katika mchezo huo wa hatua ya nusu fainali mabao ya Simba yalifungwa na Michael Fred pamoja na Israel Mwenda kwa mkwaju wa penalti.

Simba inatinga fainali ikimsubiri mshindi wa mchezo kati ya KMKM dhidi ya Azam FC ambao unatarajiwa kuchezwa leo Aprili 25 2024.