HABARI yenye mshtuko kwenye kiwanda cha Michezo na Burudani ni kutangulia mbele za haki Adel Zraine aliyewahi kuwa kocha wa viungo ndani ya kikosi cha Simba.
Kabla ya kufikwa na umauti wake alikuwa anafanya kazi na Klabu ya APR FC ya Rwanda iliyoshiriki Mapinduzi 2024.
Taarifa kutoka Klabu ya APR FC zimesema: “Ni huzuni kubwa kueleza kuwa aliyekuwa kocha wetu wa viungo Dr. Adel Zraine ametangulia mbele za haki, tunamuombea roho yake ipumzike kwa amani,”.
Mtendaji Mkuu mstaafu wa Simba, Crescentius Magori ambaye kwa sasa ni mshauri wa rais wa heshima Simba, Mo Dewji ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram: “Shocking news! RIP coach Adel Zrane.