>

NGOMA NI NZITO KIMATAIFA KETE ZA UGENINI

BAADA ya Machi 12 2024 droo ya Ligi ya Mabingwa Afrika kupangwa ambapo kila timu iliyokuwa hatua ya robo fainali ilipata fursa ya kutambua kigogo yupi atakutana naye ndani ya uwanja kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza.

Ipo wazi kwamba Simba kete yake ilikuwa dhidi ya Al Ahly ya Misri mchezo uliokuwa ukisubiriwa kwa shauku mwisho ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0-1 Al Ahly.

Simba ilipoteza mchezo wake ikiwa nyumbani Machi 29 ina kibarua cha kusaka ushindi ugenini Aprili 5 nchini Misri.

  Yanga ilianza kazi mikononi mwa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ngoma Machi 30 ilikuwa 0-0 baada ya dakika 90, Yanga inakibarua cha kusaka ushindi ugenini kati ya Aprili 5.

Matokeo ya robo fainali ya kwanza ngoma ilikuwa namna hii:-

ROBO FAINALI
Simba 0-1 Al Ahly
TP Mazembe 0-0 Petro Atletico
Esperance 0-0 ASEC Mimosas
Yanga 0-0 Mamelodi Sundowns

NUSU FAINALI
Mshindi wa mchezo wa Esperance/ASEC dhidi ya mshindi wa Yanga/Mamelodi
Mshindi wa mchezo wa TP Mazembe/Petro Atletico vs Simba/Al Ahly.

Kila la kheri wawakilishi wa Tanzania kwenye hatua hii ngumu yenye ushindani mkubwa.