WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga leo watakuwa Uwanja wa Mkapakusaka ushindi dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Kwenye mchezo wa leo mitambo ya kazi ambayo haikuwa fiti inatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi miongoni mwao ni Khalid Aucho, Pacome, Zawad Mauya huku YaoYao na Kibwana Shomari ripoti ya daktari itaamua uwepo wao.
Mastaa wa Yanga ambao walikuwa hawajaripoti kambini ikiwa ni Aziz KI na Diarra wapo kambini kamili kwa mchezo huo.
Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu lakini wapo tayari kupambana kupata ushindi.