Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo aliyechukua nafasi ya Zitto Kabwe ndani ya chama hicho, mwanamama Dorothy Semu amefunguka juu ya mjadala na maswali kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman anayetokana na ACT hana nguvu ukilinganisha na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla.
Katika mahojiano maalum kwenye Kipindi cha Front Page cha +255 Global Radio na Global TV, Dorothy anasema Makamu huyo wa Kwanza wa Zanzibar anaendelea kutekeleza majukumu yake kwa umakini mkubwa kulingana na mipaka na mfumo uliowekwa wazi na si kweli kwamba hana nguvu kama inavyoonekana…
Official Website