Mchambuzi na mwandishi nguli wa michezo, Saleh Ally amefanya mahojiano na baadhi ya waandishi wa habari na kuwaeleza kuwa kiwango alichonacho Clatous Chama mchezaji wa Simba hakilinganishwi na cha Pacome mchezaji wa Yanga.
Saleh ameendelea kuwaambia waandishi hao kuwa Chama ameipeleka Simba robo fainali mara kadhaa na amefanya makubwa sana kwa upande wa soka la Tanzania.