YANGA imeibuka na ushindi wa bao 1-0 Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Bao pekee la ushindi limefungwa na Mudathir Yahya dakika ya 86 akitumia pasi ya Kibabage.
Wakali wote wawili walitokea benchi kipindj cha pili ambapo Dodoma Jiji walikuwa wanakaribia kupata pointi moja mpango ukavurugwa jioni.
Mbinu ya Dodoma Jiji ilikuwa ni kujilinda zaidi n kushambulia kwa kushtukiza Jambo ambalo halijawapa matokeo.
Sasa Yanga inarejea nafasi ya kwanza ikiwashusha Azam FC mpaka nafasi ya pili huku Simba ikiwa nafasi ya tatu.