KAGERA SUGAR NGOMA NZITO DHIDI YA YANGA

WABABE wawili leo Februari 2 2024 wametoshana nguvu ndani ya mchezo wa Ligi Kuu kwenye msako wa pointi tatu ndani ya dakika 90.

Kwenye mchezo wa leo ambao kipindi cha kwanza timu zote zilizheza kwa kushambuliana kwa kushtukiza mabeki na makipa walikuwa kazini kutimiza majukumu yao.

Mpaka dakika 90 zinakamilika ilikuwa ni Kagera Sugar 0-0 Yanga ikiwa ni sare iliyopatikana ndani ya Februari baada ya Ligi Kuu Bara kusimama kwa muda kutokana na mashindano ya AFCON huku wachezaji wa Kagera Sugar wakionyeshwa kadi za njano kutokana na kucheza faulo pamoja na kupoteza muda.

Mbaraka Yusuph alitumia sekunde zaidi ya 20 kutoka nje wakati akifanyiwa mabadiliko huku Obrey Chirwa akijiangusha kama ilivyokuwa kwa mlinda mlango Ramadhan Chalamanda aliyeonyeshwa kadi ya njano kwenye mchezo wa leo.

Dakika 90 ubao umesoma Kagera Sugar 0-0 Yanga wakigawana poiñti mojamoja na ziliongezwa dakika 8 ambazo ilikuwa ni sawa bado zilipotezwa kizembe na Kagera Sugar wachezaji.