ANASEPA SIMBA MTAMBO WA MAPIGO HURU NTIBANZOKIZA

TAARIFA zinaeleza kuwa mtaalamu wa mapigo huru ndani ya kikosi cha Simba Saido Ntibanzokiza anasepa katika kikosi hicho kwenda kupata changamoto mpya sehemu nyingine huku mabosi wa Simba wakiwa kwenye hesabu za kumvuta kiungo mwingine wa kazi.

Nyota huyo amekuwa kwenye kiwango bora katika mechi zote anazopewa nafasi ya kuanza licha ya wengi kueleza kuwa umri umemtupa mkono.