ABDALAH Mohamed, ‘Bares’ Kocha Mkuu wa JKT Tanzania inayoshikiri Championship amesema kuwa walikwama kupata matokeo mbele ya Simba jana Desemba 14 Uwanja wa Mkapa kwa kushindwa kutumia nafasi ambazo walitengeneza.
JKT Tanzania ikiwa Uwanja wa Mkapa ilishuhudia ubao ukisoma Simba 1-0 JKT Tanzania na kuondolewa kwenye raundi ya tatu ya Kombe la Shirikisho.
Mtupiaji alikuwa ni Kibu Dennis ambaye aliweza kufunga bao hilo kipindi cha kwanza dakika ya 27 na kuipa ushindi timu ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco.
Bares amesema:”Ilikuwa tunahitaji ushindi kwa sababu mipango ya timu yangu ilikuwa vizuri kwa walichokifanya wachezaji nawapongeza licha ya kwamba tumekosa ushindi.
“Ambacho kimetokea ni kwamba wachezaji walishindwa kutumia nafasi ambazo wamezipata na mwisho wa siku tukapoteza mchezo hivyo kilichotokea ni somo kwetu kwa ajili ya mechi zijazo licha ya kwamba tumetolewa kwenye Kombe la Shirikisho,” .
Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa wachezaji wanastahili pongezi kwa kuwa walicheza kwa juhudi kwenye mchezo huo ambao ni wa mtoano kwa kuwa ukifungwa unatolewa jumlajumla.