MIGUEL Gamondi Kocha Mkuu wa Yangaameweka wazi kuwa kuna kazi kubwa ya kuongeza umakini kwenye eneo la ulinzi ili kuzuia kufungwa katika mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika. Timu hiyo baada ya kucheza mechi mbili ambazo ni dakika 180 imeokota mabao manne kwenye nyavu.