Klabu ya Simba imefanya mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kujibu maswali tofautitofauti baada ya kumtangaza Kocha wao mpya Abelhak Benchikha.
Moja ya mambo yaliyoongelewa na Benchikha ni kwamba yeye hatoangalia jina la mchezaji bali ataangalia uwezo wa kila mchezaji uwanjani ili ajue kikosi alichonacho.
Zaidi sana Benchikha amesema anataka ushirikiano kutoka kwa viongozi, wachezaji na mashabiki wa Simba.