MWILI WA MTANZANIA ALIYEFIA ISRAEL WAAGWA NYUMBANI KWA WAZAZI WAKE ROMBO KILIMANJARO – VIDEO

Mwili wa kijana Mtanzania, Clemence Felix Mtenga aliyeuawa nchini Israel kufuatia mapigano kati ya majeshi ya nchi hiyo na wapiganaji wa Hamas, umewasili nchini ambapo leo umeagwa nyumbani kwa wazazi wake, Kirwa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro huku taratibu za mazishi zikiendelea.