TUMEONA namna ambavyo wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars walivyokamilisha majukumu yao kwa kupata ushindi. Haikuwa kazi rahisi kushinda mchezo dhidi ya Niger ugenini hivyo wanastahili pongezi.
Kuanzia benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki pongezi zinawastahili kwa kuwa wamefanya kazi kubwa. Furaha ambayo wameipata wachezaji inapaswa kuwa endelevu.
Furaha ambayo wameipata mashabiki ugenini inapaswa kuwa endelevu. Bado kuna mechi ambazo wachezaji wanazo mbele wanapaswa kupambana kufanya kweli.
Wanasema haijaisha mpaka itakapokuwa imeisha hivyo ni wakati ujao kazi kubwa kupata matokeo kwenye mechi zinazoendelea.
Furaha ya muda haidumu ikiwa endelevu itakuwa ni furaha kwa mashabiki na benchi la ufundi. Kikubwa ambacho kinahitajika ni kufanya kazi kwa umakini kwenye kila mchezo.
Baada ya kumalizana na Niger kuna mchezo mwingine ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa. Kwenye mchezo huu ni muhimu kwa wachezaji kufanya kweli na kupata matokeo mazuri ndani ya uwanja.
Kuwa nyumbani na kucheza mbele ya mashabiki ni muhimu kujituma bila kuogopa.Ushindi wa pili utaongeza nguvu ya kujiamini kuelekea mechi zinazofuata.
Wachezaji wanafanya kazi kubwa hivyo inapaswa kuendelea kuwa hivyo kwenye kila mchezo.
Muda ni sasa na inawezekaa kwa wachezaji kufanya hayo kwa umakini kwa kuwa kila kitu ni maandalizi mazuri ndani ya uwanja na nidhamu.