MASTAA AZAM FC WAONGEZEWA MAUJANJA

YUSUPH Dabo, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa ni muhimu kwa wachezaji wake kuongeza umakini wakiwa kwenye mechi za ushindani ili kupata matokeo mazuri.

Timu hiyo kwenye mechi mbili za ugenini ilikomba pointi zote sita kwa sasa ipo Dar kwa maandalizi ya mchezo wake ujao wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar.

Ni pointi 19 wanazo kibindoni Azam FC sawa na Simba walio nafasi ya tatu wakiwa na tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Dabo amesema kuwa ushindani ndani ya ligi ni mkubwa hivyo wachezaji nao ni muhimu kuongeza umakini kwenye mechi zote.

“Ni ligi yenye ushindani na kila mechi ni muhimu kupata pointi tatu hivyo wachezaji wanapaswa kuongeza umakini kila wakati wawapo uwanjani kwenye kutimiza majukumu yao.

“Kwa muda ambao tunakuwa nao kwenye mazoezi kuna maendeleo ambayo yanatokea na hilo linazidi kutupa nguvu kuelekea kweye mechi zetu zinazofuata,”.