SIMBA YATAMBIA HIKI KUWAKABILI ASEC

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa utawaonyesha nguvu ya mashabiki wapinzani wao ASEC Mimosas kwa vitendo kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo.

Novemba 25 Simba inatarajiwa kucheza mchezo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Mkapa wakiwa na tuzo ya mashabiki bora wa African Fotball League.

 Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally alisema kuwa kazi kubwa kwa wachezaji ni kutafuta matokeo huku mashabiki wao wakishangilia bila kuchoka.

“Kwenye mchezo wetu dhidi ya ASEC Mimosas tunaamini kwamba mashabiki watajitokeza kwa wingi na kuonyesha nguvu tuliyonayo kwa vitendo. Tumetoka kushinda tuzo ya African Football League upande wa mashabiki hivyo sasa tunakwenda kuonyesha kwa vitendo.

Tunawaheshimu wapinzani wetu na tunatambua kwamba utakuwa ni mchezo mgumu kwa kuwa ni mchezo muhimu. Hivyo mashabiki tushikamane na tuwaongezee nguvu ile ya mchezaji wa 12 wachezaji,” alisema Ally.