AZIZ KI kiungo wa Yanga ni kiboko yao kwa makipa wote namba moja ndani ya timu zilizo tatu bora kwa kuwa kawatungua kwenye mechi za ligi walipokutana.
Nyota huyo katupia jumla ya mabao saba kibindoni akiwa na pasi moja ya bao kwa msimu wa 2023/24 ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.
Kwenye mabao yake saba aliyonayo mguu wake wenye nguvu ni ule wa kushoto ambapo katupia mabao matano huku ule wa kulia akitupia mabao mawili.
Ni Idrisu Abdulai kipa namba moja wa Azam FC iliyo nafasi ya pili kwenye msimamo alikutana na balaa la Aziz KI alipotunguliwa jumla ya mabao matatu.
Katika mchezo huo wa Mzizima Dabi KI aliandika rekodi ya kumtungua Abdulai mabao hayo ilikuwa dakika ya 8, 69 na 71 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 3-2 Azam FC ilikuwa ni Oktoba 23.
Kivumbi kiliwaka ubao wa Uwanja wa Mkapa uliposoma Simba 1-5 Yanga ilikuwa Novemba 5 2023. KI alimtungua Aishi Manula bao moja dakika ya 73.
Simba iliyo nafasi ya tatu na Azam FC zote ziliacha pointi sita kwa Yanga inayoongoza ligi huku makipa wote wakiwa hawana bahati ya kuachwa salama