COASTAL UNION WAPOTEZA POINT MBELE YA YANGA

CLEMENT Mzize mshambuliaji wa Yanga amefunga bao lake la kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24.

Bao hilo ni muhimu kwa Yanga kwa kuwa wamekomba pointi tatu mazima ugenini.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkwakwani umesoma Coastal Union 0-1 Yanga.

Bao hilo limejazwa kimiani dakika ya 70 kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa huku langoni akianza Aboutwalib Mshery.

Katika mchezo wa leo kulikuwa na mabadiliko kwenye kikosi cha kwanza cha Miguel Gamond kutokana na wachezaji hao kutoka kucheza mchezo mgumu wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba na kushuhudia ubao ukisoma Simba 1-5 Yanga.