BAADA ya Simba kugotea hatua ya robo fainali African Football League, mkongwe kwenye masuala ya uandishi wa habari za kimicheza Jembe ametaja sababu ya timu hiyo kukwama kusonga mbele.
Jembe ameanza kwa kuuliza namna hii:-Unataka uilamu Simba kwa sare ya 1-1 Vs Al Ahly hapa Cairo?
Ahly umeisahau? Huujui ukubwa wake? Leo mashabiki wake kwenye Uwanja wa Cairo International Stadium wameipigia Simba makofi ya pongezi.
Yes, Simba wameonyesha ukubwa wa uwezo wa kupambana na timu kubwa lakini wametolewa.
Sare ya 2-2 Dar na sasa 1-1 Cairo. Haijapoteza mchezo lakini kanuni inawaadhibu.
Simba hawapaswi KUSIKITIKA, wanapaswa kujifunza kwa sababu matokeo ya Cairo ni sahihi lakini shida ni matokeo ya Dar es Salaam…
Mara nyingi Simba inatolewa hatua ya robo fainali baada ya kushindwa kufanya vizuri Dar es Salaam.
Iwe inaanzia ugenini au nyumbani, mara nyingi Simba inakosea Dar es Salaam.
Hapa ndipo wanapaswa kubadilika ili wavuke hatua ya robo fainali…
Kwa hapa Cairo, tuwapongeze….kazi ngumu wameifanya ionekane inawezekana lakini Dar es Salaam IMEWAHARIBIA…sababu hawaitumii vizuri..
Leo si muda wa kupaniki, Simba haijawaabisha mashabiki wake na Watanzania kwa ujumla lakini imetoka na hili ndio muhimu zaidi.
Ninaamini ni SOMO SAHIHI na kwa wakati kwenda Caf Champions League hatua ya MAKUNDI..