KOCHA mpya wa Singida Fountain Gate, Ricardo Ferreira kutoka Brazil ana kete nne ngumu kusaka pointi 12 kwenye mechi zake za mwanzo ndani ya timu hiyo.
Ikumbukwe kwamba kocha huyo anakuja kuchukua mikoba ya Ernst Middendorp aliyekiongoza kikosi hicho kwenye mchezo mmoja dhidi ya Future uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Septemba 18.
Katika mechi hizo nne ambazo ni dakika 360, Ferreira ni mchezo mmoja pekee atakuwa nyumbani Uwanja wa Liti dhidi ya Ihefu unatarajiwa kuchezwa Novemba Mosi.
Ni mechi tatu anatarajiwa kukutana na vigogo vya kusaka pointi tatu ugenini itakuwa dhidi ya Namungo Oktoba 21, Uwanja wa Majaliwa, Yanga Oktoba 26 Uwanja wa Azam Complex.
Kete ya nne Mbrazil atakuwa Kigoma mwisho wa reli kumenyana na Mashujaa itakuwa ni Novemba 6, Uwanja wa Lake Tanganyika.