GEITA GOLD WAPOTEZA MBELE YA YANGA

GEITA Gold wamepishana na pointi tatu kwa mara nyingine kwenye mchezo wa pili mfululizo baada ya kupoteza mbele ya Yanga.

Mchezo uliopita Geita Gold ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Nyankumbu ukisoma Geita Gold 1-2 KMC.

Baada ya dakika 90 kwenye mchezo wa leo Oktoba 7 ubao wa Uwanja wa Kirumba umesoma Geita Gold 0-3 Yanga.

Kazi ya Yanga ilianza dakika ya 44 kupitia kwa Pacome aliyepachika bao dakika ya 44 na bao la pili ni mali ya Aziz Ki aliyepachika bao hilo dakika ya 45.

Kipindi cha kwanza Yanga walikuwa mbele kwa mabao mawili na waliporejea waliongeza bao moja.

Maxi Nzengeli alipachika bao la tatu lililoipa pointi tatu Yanga ikiwa ugenini.