SIMBA YAWAVUTIA KASI POWER DYNAMOS LIGI YA MABINGWA AFRIKA

BAADA ya kutoshana nguvu mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa wakiwa ugenini, hesabu za Simba ni kupata ushindi mchezo ujao.

Ubao wa Uwanja wa Levy Mwanawasa baada ya dakika 90 ulisoma Power Dynamos 2-2 Simba.

Mabao yote ya Simba yalifungwa na kiungo Clatous Chama ambapo lile la kuweka usawa alifunga dakika ya 90 muda mfupi kabla ya mpira kugota mwisho.

Chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira wachezaji wa Simba wameanza mazoezi katika Uwanja wa Mo Simba Arena uliopo Bunju.

Miongoni mwa wachezaji hao ni pamoja na Kibu Dennis, Willy Onana, Luis Miquissone na Jean Baleke.

Septemba 26 kikosi cha Simba kilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Pan African inayoshiriki Championship ikiwa ni kujiweka fiti kuelekea mchezo wao na ilipata ushindi wa mabao 4-0.

Mchezo ujao dhidi ya Power Dynamos unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, Oktoba Mosi.